Maombi
- Maombi yanajumuisha Fomu ya Maombi, Wazo la Biashara na Hati ya Mkataba. Haya yatatakiwa kujazwa na kuwasilishwa kwa mkono kupitia Ofisi za Mikoa za SIDO/ZNCCIA (Unganisha) au kwa intaneti kupitia mtandao wa Business Development Gateway.
- Mombi kwa ajili ya Mashindano ya Mpango wa Biashara, 2009 yawasilishwe Kati ya Tarehe 15 Januari, 2009 – 25 Februari, 2009. Maombi yatakayochelewa hayatafikiriwa.
- Mshiriki atawasilisha wazo moja tu katika Mashindano ya Mpango wa Biashara, 2009.
- Baada ya Wazo la Biashara kuwasilishwa halitaweza kuondolewa tena.
- Wazo la biashara litatakiwa kuwa wazo binafsi la Mshiriki.
- Wazo la Biashara liandikwe katika Muhtasari wa kurasa 2 – 3
- Waombaji ni lazima wafuate masharti ya Mashindano ya Mpango wa Biashara. Maelezo ya Masharti yamewekwa ndani ya Kifurushi cha Taarifa kwa Washirik ikinachopatikana Ofisi za SIDO/ZNCCIA
- Wazo la Biashara ni lazima lichapwe katika Microsoft Word in Times New Roman, font size 12. Maombi yaliyoandikwa kwa mkono hayatafikiriwa.
- Ada ya ushiriki kwenye mashindano ni Tzs 10,000/=. Ada hii italipwa na Wajasiriamali watakaochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya kwanza. Ada inaweza kulipwa kwa fedha Taslim au kwa kuwekwa Benki ya NMB au PBZ na Hati ya Kuweka fedha Benki kuonyeshwa.
- Washiriki ni lazima wakubali masharti ya Mashindano na kuweka saini Hati ya Mkataba wa Ushiriki wakati wanashiriki kwenye mafunzo ya mwanzo ya Mashindano ya Mpango wa Biashara.
- Washiriki waliochaguliwa kushiriki katika mashindano watatakiwa wao binafsi kuhudhuria kwenye mafunzo na kuwasilisha mipango yao.
Zawadi
- Washiriki ni lazima wawe na Akaunti au wawe tayari kufungua Akaunti NMB, kwa washiriki wa Tanzania Bara, au Benki ya Watu wa Zanzibar, PBZ, kwa washiriki wa Zanzibar. Akaunti hizi zitatumika kupokelea zawadi kwa Washiriki watakaoshinda.
- Zawadi za Mashindano haziwezi kuhamishwa, kulipwa kupitia mtu mwingine na kuongezewa muda.
- Zawadi zitatolewa kulingana na Sheria za Tanzania, ikiwa ni pamoja na Sheria za Kodi.
- Zawadi za fedha ni kwa ajili ya shughuli za biashara. Washiriki watakaopata zawadi watalazimika kuweka saini Fomu ya Matumizi ya Zawadi.
Utunzaji wa Siri
- Majaji, Wafadhili, Waongozaji na Washauri wa Biashara watakaohusika na Mashindano ya Mpango wa Biashara watatunza siri zote kuhusu mawazo na mipango ya biashara. Hata hivyo, ni juu ya Washiriki wenyewe kutunza miliki ya mawazo yao ya biashara.
- Maingizo yote katika Mashindano ni mali ya Waombaji.
- Taarifa za Usajili na Taarifa Binafsi za Washiriki zitaweza kutumiwa kwa ajili ya kumbukumbu na promosheni.
Lugha
- Hatua zote za Mashindano ya Mpango wa Biashara zitakuwa kwa Kiingereza, ikiwa ni pamoja na, uwasilishaji wa wazo na mpango wa biashara na uwasilishaji kwa maelezo katika hatua ya fainali ya mashindano. Hata hivyo, Wakufunzi watatumia lugha zote, Kiswahili na Kiingereza wakati wa mafunzo.






