The Business Plan Competition consists of a number of phases:
Hatua ya 1: Maombi na Uchambuzi
Washiriki wataomba kushiriki katika Mashindano ya Mpango wa Biashara kati ya tarehe 15 Januari mpaka 25 Februari, 2009. Maombi yanaweza kuwasilishwa kwa intaneti kupitia mtandao wa Business Development Gateway au kwa mkono kupitia ofisi za Mikoa za SIDO/ZNNCIA.
Maombi yote yatafanyiwa uchambuzi ili kuhakikisha yanatimiza masharti na sheria za Mashindano. Mawazo yote ya Biashara yatafanyiwa tathmini na Timu ya Majaji. Wajasiriamali 500 wenye mawazo mazuri zaidi ya biashara wataalikwa kushiriki katika mafunzo.
Hatua 2: Mafunzo ya Ujasiriamali na Mpango wa Biashara
Mwezi Machi, 2009 Wajasiriamali 500 wenye mawazo mazuri zaidi ya biashara watashiriki katika mafunzo ya siku moja yatakayoendeshwa Mikoani. Mafunzo yatawapa Washiriki elimu na ujuzi ambao wanaweza kuutumia kuboresha mawazo yao ya biashara na kutengeneza muhtasari wa biashara. Baada ya mafunzo, Washiriki watarekebisha mawazo yao ya biashara na kuwasilisha Muhtasari wa Biashara. Timu ya Majaji itafanyia tathmini mihtasari iiyowasilishwa na mihtasari bora zaidi 250 itachaguliwa na kupewa zawadi ya fedha, Dola za Marekani 2,500/= kwa kila muhtasari ulioshinda.
Hatua 3: Kutayarisha Mpango wa Biashara
Washindi 250 wa Hatua ya 2 wataalikwa kwenye mafunzo ya siku 3 ya Utayarishaji wa Mpango wa Biashara yatakayoendeshwa Makao Makuu ya Mkoa. Mafunzo yatalenga mada zote za Ujasiriamali, ikiwa ni pamoja na, fedha, masoko, uzalishaji na usimamizi wa wafanyakazi. Mafunzo yatawasaidia Washiriki kurekebisha na kuboresha Mipango yao ya Biashara. Mpango wa mwisho wa Biashara utawasilishwa Mei, 2009. Timu ya Majaji itafanyia tathmini Mipango yote ya Biashara na Mipango bora zaidi 50 itachaguliwa. Washindi hawa 50 kila mmoja atapewa zawadi ya Dola Za Marekani 7500/=
Hatua 4: Mafunzo ya Biashara na Ushauri
Washindi 50 wa Hatua ya 3 wataalikwa kushiriki Warsha ya Mafunzo ya siku 5 ya ndani zaidi kuhusu mada za utayarishaji wa Mipango ya Biashara, Menejimenti na ushauri wa mtu mmoja mmoja. Mafunzo yatatoa fursa kwa Washiriki kuboresha Mipango yao ya Biashara kwa msaada wa Mshauri wa Biashara. Baada ya kuwasilisha Mpango uliofafanuliwa wa Biashara, washindi 50 watawasilisha maelezo ya mdomo Mipango yao ya Biashara kwa Timu bora zaidi ya Majaji mwezi Juni, 2009. Baada ya mawasilisho ya Mipango ya Biashara na mawasilisho ya mdomo, Majaji watafanya tathmini na kuchagua washindi 5. Washindi hawa 5 watapata zawadi za fedha kuanzia Dola za Marekani 10,000/= mpaka 15,000/= zitakazotolewa kwa Mshindi wa kwanza kwa Mashindano ya Mpango wa Biashara, 2009.
Huduma baada ya Mashindano
Wajasiriamali 50 waliofikia fainali ya Masindano ya Mpango wa Biashara wategemee kuendelea kupata msaada kutoka kwa Washauri ambao watawapa taarifa muhimu, kuwaunganisha na Taasisi za Fedha na Watoa Huduma mbalimbali za Biashara na Vyama vya Wafanyabiashara.
Washiriki wote 250 wa Hatua ya 2 wataalikwa kwenye Hafla ya Washiriki wa Mashindano ya Mpango wa Biashara. Hafla hii itawapa fursa ya kukutana na Wajasiriamali wengine ili kubadilishana uzoefu na kujenga mtandao wa jamii ya wafanya biashara nchini Tanzania.
