Nani wanaweza kushiriki?

Unaweza kushiriki katika Mashindano ya Mpango wa Biashara ikiwa:
  • Ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na unaishi au kufanya kazi Bara, Zanzibar au Pemba.
  • Utaomba kama mshiriki binafsi.
  • Una umri wa miaka 18 au zaidi.
  • Wazo lako la Biashara linatekelezeka, ni halali na linahusu upanuzi wa biashara iliyopo au uanzishaji wa biashara mpya nchini Tanzania.
  • Una biashara iliyosajiliwa yenye kulenga kupata faida au unakusudia kusajili biashara yenye kulenga kupata faida.
  • Una biashara yenye umiliki binafsi. Iwapo ni biashara ya ubia, basi wamiliki wenye Hisa kubwa zaidi wawe Watanzania.
  • Wazo lako la biashara liwe katika sekta zifuatazo: Biashara ya Kilimo na Usindikaji, Uzalishaji Kiwandani, Utalii au Huduma (Bonyeza ili kuona mifano).
Hutaweza kushiriki katika Mashindano ya Mpango wa Biashara ikiwa:
  • Ni Jaji, Mkufunzi, Mtaalamu au Mtumishi wa Business Development Gateway au mojawapo ya Asasi Shiriki.
  • Ulipata zawadi katika Mashindano yaliyopita ya Mpango wa Biashara (Ikiwa ni pamoja na 2007 Bid Challenge, 2007 and 2008 UDEC and TechnoServe Competitions)
  • Unataka kushiriki kama Kampuni au vinginevyo (ni wajasiriamali binafsi tu wanaoweza kushiriki).
  • Biashara yako inamilikiwa kwa kiasi kidogo au kikubwa au ina dalili za kumilikiwa na kuendeshwa na Serikali ya Tanzania au Serikali ya Zanzibar.
  • Una biashara isiyolenga kupata faida.
  • Biashara yako au Wazo lako la Biashara lipo katika Sekta isiyokuwa kwa mfano, biashara, kilimo cha kujikimu, ufugaji wa wanyama, biashara ya bidhaa za kilimo zisizosindikwa, udalali katika Utalii, kuendesha nyumba za kulala wageni au huduma zisizoongeza thamani mfano, Ushauri, Masoko na Utaalamu.

Mifano

Mfano wa Biashara za Viwandani
  • Kutengeneza Matofali
  • Bidhaa za ngozi ya wanyama
  • Utengenezaji Chokaa
  • Vinyago
  • Ufinyanzi
  • Nguo
  • Useketaji
  • Kuweka rangi nguo
  • Samani
  • Bidhaa za Makanika
  • Sabuni za Miche na Unga
  • Utengenezaji wa Vyuma
  • Na zingine nyingi...
    • Mifano ya Biashara za Kilimo na Usindikaji
      • Kusindika asali
      • Matunda na juisi ya matunda
      • Samaki na Usindikaji bidhaa za Baharini
      • Usindikaji wa Bidhaa za Wanyama
      • Mvinyo
      • Usindikaji wa Karanga
      • Bidhaa za Mifugo
      • Na zingine nyingi...
      Mifano ya Biashara za Utalii
      • Utalii wa Baharini
      • Ubunifu wa Utalii unaolenga soko la ndani na nje
      • Kusindika bidhaa zinazolenga soko la Utalii
      • Na zingine nyingi...
      Mifano ya Biashara za Huduma
      • Elimu
      • Afya
      • Huduma za Mifugo
      • Utoaji wa Huduma Bunifu za Teknolojia ya Mawasiliano (ICT)
      • Na zingine nyingi...

      The competition rules

HOME | SITEMAP | CONTACT | All information and services on this site © 2009 TPSF | Site by TTC