Unakaribishwa kushiriki katika Shindano la Kitaifa la Mpango wa Biashara (BPC) mwaka 2010-2012, inayoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafi Tanzanaia-Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) kupitia Programu ya Business Development Gateway (BDG)-Fanikiwa Ki-biashara. Kabla ya kuendelea hakikisha kwamba unatimiza mambo yafuatayo:
- ninalo wazo la biashara linalotekelezeka
- ninapenda kuongeza elimu na ujuzi wangu wa biashara
- nipo tayari kutumia ushauri wa Wataalamu wa biashara
- Ninahitaji fedha za mtaji wa kutekelezea wazo langu la biashara
Mashindano ya Mpango wa Biashara (BPC) yanawasaidia Wajasiriamali wa Kitanzania waliopo na wanaopenda kutekeleza mawazo yao ya biashara na pia yanawapa fursa kushiriki katika mafunzo ili kuongeza elimu na ujuzi wa biashara. Kwa wale watakaojiunga na BPC kuna nafasi ya kushinda moja ya zawadi za fedha zaidi ya 400 zinazoanzia Dola za Marekani 2,000/= mpaka 16,000/=.






