Sheria

Usajili/Maombi

  • Kifurushi cha Usajili/Maombi kina Fomu ya Usajili masharti na sheria za ushiriki.
  • Waombaji watakaoteuliwa kushiriki watapewa kifurushi cha Taarifa chenye Fomu ya Taarifa ya Biashara, Sheria za BDP na Hatiya Mkataba. Fomu hizi zitatakiwa kujazwa, kusainiwa na kuwasilishwa kwa mkono kupitia Ofisi za Mikoa za SIDO/ZNCCIA au kupitia mtandao wa Business Development Gateway.
  • Kipindi cha Maombi ni kati ya tarehe 15 January mpaka 6 Februari 2009. Maombi yatakayochelewa hayatafikiriwa.
  • Ada ya maombi ni shs. 5,000/=. Ada hii italipwa na Wajasiriamali waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya kwanza. Ada inaweza kulipwa kwa fedha taslim.
  • Wajasiriamali watakaochaguliwa kushiriki katika Programu ya BDP ni lazima wao binafsi wawepo katika vituo vya mafunzo kuhudhuria mafunzo.

Zawadi

  • Washiriki wawe na Akaunti au wawe tayari kufungua Akaunti ya Benki kwa ajili ya kupokelea zawadi. Akaunti zifunguliwe Benki ya NMB kwa washiriki kutoka Tanzania Bara au PBZ kwa Washiriki kutoka Zanzibar na Pemba.
  • Zawadi zitakazotolewa haziwezi kuhamishiwa kwa mtu mwingine, kulipwa kupitia mtu mwingine na kuongezewa muda.
  • Zawadi zitatolewa kulingana na Sheria za Tanzania, ikiwa ni pamoja na Sheria za Kodi.
  • Zawadi zitatumika kwa ajili ya shughuli za biashara. Washiriki wanaopata zawadi wataombwa kujaza na kusaini Fomu ya Matumizi ya Zawadi.

Utunzaji wa Siri

  • Washauri na waandaaji wa Programu ya BDP ni Wataalamu wanaoheshimika sana na kila siku wanafanyia kazi taarifa nyingi za siri. Watatunza taarifa zote za siri.
  • Washiriki ni lazima wakubali kutoas taarifa za biashara zao na kukubali kwamba taarifa za usajili na taarifa binafsi zinaweza kutumika kwa kumbukumbu na promosheni ya Programu.

Lugha

  • Lugha za Kiingereza na Kiswahili zitatumika katika Progamu hii. Kiswahili kitatumika katika uendeshaji wa mafunzo.

How will your business be evaluated?

HOME | SITEMAP | CONTACT | All information and services on this site © 2009 TPSF | Site by TTC