Hatua

Hatua 1: Usajili na mapokezi

Washiriki wataomba kushiriki katika Programu ya BDP kati ya tarehe 15 January na 6 February, 2009. Hii inajumuisha kujaza Fomu ya Usajili, Kujaza Fomu ya Taarifa za Biashara na Hati ya Mkataba.

Usajili unaweza kufanyika kupitia mtandao wa Business Development Gateway au kwa mkono kupitia ofisi za Mikoa za SIDO/ZNCCIA. Maombi yote yatachambuliwa kuona kama yametimiza masharti na sheria za Ushiriki.

Hatua 2: Warsha za Uanzilishi na Mafunzo ya 1 ya Uendelezaji Ujasiriamali

Washiriki wote walioteuliwa na kuwasilisha Fomu ya Taarifa ya Biashara wataalikwa kuhudhuria Warsha ya Uanzilishi na mafunzo ya Uendelezaji Ujasiriamali yatakayofanyika Mkoani. Wakati wa Warsha washiriki watapata nafasi ya kujadiliana changamoto katika biashara zao. Mafunzo yanalenga katika kufundisha ujuzi na elimu ya biashara na yanajumuisha mikakati na utayarishaji wa mipango ya biashara. Washauri wenye uzoefu watawasaidia washiriki kutambua hatua muhimu zinazolenga utayarishaji wa Mpango binafsi wa Biashara.

Miezi miwili itakayofuata baada ya mafunzo, Washiriki watapata nafasi kutayarisha Mpango wa Biashara. Wataombwa kujaza na kuwasilisha Fomu Binafsi ya Kujipima Na. 1 ikionyesha matokeo ya hatua zilizotekelezwa. Uwasilishaji wa Fomu Binafsi za Kujipima unapendekezwa ufanyike kwa mkono kupitia Ofisi za Wawakilishi wa BDG zilizopo Mikoani (Ofisi za SIDO/ZNCCIA) au kupitia mtandao wa BDG. Wataalamu Washauri watazifanyia tathmini fomu Binafsi za Kujipima na kuwapa Wajasiriamali alama za bonasi iwapo biashara zao zitakuwa zimeonyesha maendeleo. Washiriki wote wataarifiwa kuhusu matokeo ya tathmini kutoka kwa Washauri.

Hatua 3: Mafunzo ya 2 ya Uendelezaji Ujasiriamali

Wajasiriamali wote waliowasilisha Fomu Binafsi za kujipima wataalikwa kwenye mafunzo ya siku moja ya Uendelezaji Ujasiriamali yatakayoendeshwa Mikoani. Mafunzo yatalenga soko, masoko na huduma kwa wateja. Katika mafunzo haya Washiriki wataweka pamoja hatua kamili za kutekeleza ndani ya Mipango yao ya Biashara ili kuboresha biashara zao.

Miezi miwili inayofuata baada ya mafunzo Washiriki watapata fursa ya kutekeleza mambo waliyopanga. Wataombwa kujaza na kuwasilisha Fomu Binafsi ya Kujipima Na. 2 kuonyesha matokeo ya hatua zilizotekelezwa. Uwasilishaji wa Fomu Binafsi za Kujipima unapendekezwa ufanyike kwa mkono kupitia Ofisi za Wawakilishi wa BDG Mikoani (Ofisi za SIDO/ZNCCIA) au kupitia mtandao wa BDG. Washauri wataalamu wa Biashara watazifanyia tathmini Fomu Binafsi za Kujipima na kuwapa Wajasiriamali alama za bonasi iwapo biashara imeonyesha maendeleo. Wajasiriamali watapewa taarifa kuhusu matokeo ya tathmini hii kutoka kwa Washauri.

Hatua 4: Mafunzo ya 3 ya Uendelezaji Ujasiriamali

Wajasiriamali wote waliowasilisha Fomu Binafsi ya Kujipima wataalikwa kwa mafunzo mengine ya siku moja kuhusu Uendelezaji Ujasiriamali. Mafunzo yatafanyika Mkoani na yatalenga usimamizi wa uzalishaji na ununuzi. Wakati wa mafunzo washiriki wataingiza hatua mahsusi za kutekeleza ndani ya Mipango yao ya Biashara ili kuboresha biashara zao. Miezi miwili inayofuata, Washiriki watatekeleza Mipango yao. Wataombwa kujaza na kuwasilisha Fomu Binafsi za Kujipima na 3 kuonyesha matokeo ya utekelezaji wa Mipango yao. Uwasilishaji wa Fomu binafsi za Kujipima unapendekeza ufanyike kupitia Ofisi za Wawakilishi wa BDG Mikoani (Ofisi za SIDO/ZNCCIA) au kwa kupitia mtandao wa BDG. Washauri Wataalam wa Biashara watazipitia Fomu Binafsi za Kujipima, watatoa alama za bonasi kwa biashara zilizoonyesha maendeleo na kutoa mrejesho kwa Wajasiriamali.

Hatua 5: Mafunzo ya 4 ya Uendelezaji Ujasiriamali na Upimaji wa Mwisho wa Biashara

Wajasiriamali wote waliowasilisha Fomu Binafsi za Kujipima wataalikwa kwenye mafunzo ya mwisho Mkoani. Mafunzo haya yatalenga katika Usimamizi wa Fedha ikiwa ni pamoja na Utunzaji wa kumbukumbu na uhasibu, usimamizi wa fedha, gharama na upangaji bei na utayarishaji wa taarifa za fedha.

Wakati wa mafunzo Washiriki wataingiza hatua mahsusi za kuchukua katika Mipango yao ya biashara ili kuendeleza biashara zao. Miezi miwili baada ya mafunzo washiriki watapata nafasi kutekeleza hatua walizopanga katika Mipango yao ya Biashara.

Wataombwa kujaza na kuwasilisha Fomu Binafsi ya Kujipima Na. 4 kuonyesha matokeo ya hatua zilizotekelezwa. Uwasilishaji wa Fomu Binafsi za Kujipima unapendekezwa ufanyike kwa mkono kupitia ofisi za Wawakilishi wa BDG mkoani (Ofisi za SIDO/ZNCCIA) au kwa mtandao kupitia mtandao wa BDG. Washauri Wataalamu wa Biashara watazifanyia tathmini Fomu Binafsi za Kujipima na kuzipa alama za bonasi. Biashara zote zilizoonyesha kupiga hatua ya maendeleo. Wajasiriamali watapewa taarifa ya tathmini iliyofanyika. Washauri watajumlisha alama za bonasi zilizopatikana kwa kila mshiriki. Jumla ya alama za bonasi zitaamua aina ya zawadi ambayo kila Mshiriki atapata; zawadi zinaweza kufikia kiwango cha juu cha Dola za Marekani 1000/= kwa kila Hatua.

HOME | SITEMAP | CONTACT | All information and services on this site © 2009 TPSF | Site by TTC