Unaweza kushiriki katika Programu ya BDP iwapo:
- Ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na unaishi/unafanya kazi Tanzania Bara, Zanzibar au Pemba.
- Una umri wa miaka 18 au zaidi.
- Unaomba kama mtu binafsi.
- Una biashara yenye maendeleo madogo na/au biashara isiyo rasmi.
- Biashara yako inamilikiwa binafsi.
- Biashara yako inalenga kupata faida.
- Iwapo biashara yako ni ya ubia, Watanzania wanamiliki zaidi ya 51% ya Hisa.
- Biashara yako inamiliki au inakodisha sehemu ya biashara.
- Biashara yako ina umri unaozidi mwaka mmoja (lakini si lazima iwe imesajiliwa).
- Biashara yako ipo katika Sekta zifuatazo:
Biashara ya Kilimo na Usindikaji, Uzalishaji Viwandani, Utalii au Huduma. (Angalia mifano ya biashara hizi).
- Unafahamu vizuri Kiswahili (kuongea, kusoma na kuandika; kujua Kiingereza ni sifa ya Ziada.
Hutaweza kushiriki katika Programu ya BDP iwapo:
- Wewe ni Jaji, Mkufunzi, Mshauri au Mfanyakazi wa Business Development Gateway au Asasi Shiriki.
- Unashiriki kama Kampuni au Asasi ingine (Washiriki ni lazima wawe watu binafsi).
- Biashara yako inamilikiwa kwa kiasi chochote au ina dalili zozote za kumilikiwa au kuendeshwa na Serikali ya Tanzania.
- Biashara yako haikusudii kupata faida.
- Biashara yako au wazo la biashara yako halipo katika sekta inayokua, ikiwa ni pamoja na biashara, kilimo cha kujikimu, biashara katika bidhaa za kilimo zisizosindikwa, udalali katika Utalii, nyumba za wageni au huduma zisizoongeza thamani mfano, Ushauri, Masoko na Ushauri.
- Biashara yako inahusisha uzalishaji wa silaha, vinywaji vyenye kileo, tumbaku au kamari.
Mifano
Mifano ya biashara za Uzalishaji Kiwandani:
- Kutengeneza Matofali
- Bidhaa za ngozi ya wanyama
- Kutengeneza chaki
- Vinyago
- Ufinyanzi
- Kuseketa
- Kuwepa rangi nguo
- Samani
- Bidhaa za Makenika
- Sabuni za miche na unga
- Kutengeneza kazi ya vyuma
- Na zingine nyingi...
Mifano ya Biashara za Kilimo na Usindikaji
- Kusindika asali
- Kusindika matunda na juisi ya matunda
- Upangaji wa Gredi na Ufungaji wa Mazao ya punje yasiyoharibika
- Samaki na Usindikaji wa mazao ya bahari
- Usindikaji wa mazao ya wanyama
- Mvinyo
- Kusindika karanga
- Mazao ya ufugaji
- Na zingine nyingi...
Mifano ya Biashara katika Utalii
- Utalii wa Bahari
- Ubunifu unaolenga utalii wa ndani na nje
- Usindikaji wa Bidhaa kwa soko la Utalii
- Na zingine nyingi...
Mifano ya Biashara za Huduma:
- Elimu
- Afya
- Huduma za Wanyama
- Utoaji wa Huduma Bunifu katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
- na zingine nyingi...