Zawadi

Lengo kuu la Programu ya Kuendeleza Biashara (BDG) ni kuwapa Wajasiriamali wa Kitanzania fursa ya kupata mafunzo ya ujuzi na elimu ya biashara na kuwapa ushauri utakaowasaidia kuendeleza biashara zao. Wajasiriamali wote watakaoshiriki na kuonyesha maendeleo katika biashara zao watapewa zawadi za fedha ili kuwekeza katika biashara zao.

Kwa kifupi, Wajasiriamali wote washiriki:

  • Watapata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ambayo yataboresha ujuzi na elimu yao ya biashara.
  • Watapata nafasi kujadiliana changamoto za biashara zao na Washiriki wenzao na Washauri Wataalamu ili kupanga hatua za kuchukua kuboresha biashara zao.
  • Wataweza akupata zawadi za fedha mpaka kufikia Dola za Marekani 1000/= kwa kila hatua.

HOME | SITEMAP | CONTACT | All information and services on this site © 2009 TPSF | Site by TTC