Unakaribishwa kushiriki katika Business Diagnostic Programme (BDP) Awamu ya Nne 2011/2012. Programu hii inaendeshwa na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania kupitia Programu ya Kufanikiwa Kibiashara. Kabla ya kuendelea, hakikisha unatimiza mambo yafuatayo:
- Biashara yangu si kubwa na haijasajiliwa, ila ninapenda ikue na ifanikiwe zaidi.
- Biashara yangu imesajiliwa ila haina leseni lakini bado ninapenda kufanikiwa zaidi.
- Ninapenda kuendeleza elimu na ujuzi wangu wa biashara.
- Nipo tayari kutumia ushauri wa kibishara.
- Ninahitaji mtaji wa fedha ili kutekeleza mawazo yangu na kuendeleza biashara yangu.
Kama mambo yote yanakuhusu, basi upo katika sehemu sahihi. BDP inawapa Wajasiriamali wa Kitanzania zana muhimu za kujipima, mafunzo ya biashara na ushauri ili kuzibadilisha biashara kuwa kubwa na zenye mafanikio zaidi. Programu inalenga biashara ndogo na/au ambazo si rasmi.
Hii ina maana kwamba biashara yako haihitaji kuwa imesajiliwa ili uweze kushiriki katika BDP na kufaidika na mafunzo ya biashara. Wajasiriamali wote watakaoonyesha maendeleo katika biashara zao na kutekeleza kwa mafanikio elimu na ujuzi watakaoupata wakati wa kuendesha Programu, watapata zawadi zinazoweka kufika Dola za Marekani 800 mwisho wa hatua ya nne ya mafunzo.






