Maelezo ya Utangulizi
BDG ni sehemu ya Programu ya Kushindanisha Sekta Binafsi (Private Sector Competitiveness Programme – PSCP). Katika mpango mkubwa wa PSCP Serikali ya Tanzania inalenga kuboresha Sekta Binafsi nchini Tanzania.
PSCP ina malengo makuu matatu yafuatayo:
- Kuboresha mazingira na utoaji wa huduma za kiserikali kwa Sekta binafsi kupitia Programu ya Business Environment Strengthening for Tanzania (BEST).
- Kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa biashara ndogo na za kati kupitia Financial Sector Deepening Trust.
- Kuongeza ushindani wa biashara za Kitanzania kupitia Cluster Competitiveness Programme, Matching Grants Programme na Business Development Gateway.
Mfadhili wa BDG
BDG itasimamiwa na Tanzania Private Sector Foundation. BDG itaendeshwa nchi nzima kwa kushirikiana na Washiriki 5 wafuatao:
National Microfinance Bank NMB
NMB ni Benki kubwa kuliko zote Tanzania. Ikiwa na matawi zaidi ya 120, NMB inatoa huduma za kifedha kwa wateja nchini kote. NMB ni Mshirika Mkuu Tanzania Bara katika utoaji wa zawadi za fedha na misaada na kutoa huduma za kifedha kwa washiriki wa Business Plan Competition (BPC) na Business Diagnostic Programme (BDP).
NMB website: www.nmbtz.com
The Peoples Bank of Zanzibar
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ni Mshirika Mkuu wa BDG, Tanzania Zanzibar. PBZ inatoa huduma katika Mikoa yote ya Zanzibar na ni Mshirika Mkuu katika kutoa zawadi za fedha na misaada na huduma za kifedha kwa washiriki wa BPC na BDP.
ZAIN
Zain gives you reliable mobile phone service. And, as always, we are committed to making life better for people in Tanzania.
Our mobile phone networks help businesses, communities and families stay in touch.
ZAIN website: www.tz.zain.com
Washiriki wakuu wa BDG
TCCIA
Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) kina ofisi za Mikoa katika Mikoa 21 Tanzania Bara. Ofisi hizi zinajitegemea katika shughuli zao. Ofisi hizi za TCCIA ni kiungo cha Sekta Binafsi naa Serikali ili kuboresha utendaji wa Sekta binafsi. TCCIA itatoa huduma za kuitangaza BDG.
TCCIA website: www.tccia.co.tz
Small Industries Development Organisation SIDO
Shirika la Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO) lina uzoefu wa muda mrefu wa utoaji huduma za kibishara kwa biashara ndogo na za kati nchini Tanzania. SIDO inatoa huduma nyingi, kuanzia mafunzo ya biashara na ushauri katika utumiaji wa teknolojia mpya na uboreshaji wa teknolojia na huduma za kifedha.
Ikiwa na mtandao wa ofisi uliosambaa nchi nzima, SIDO ni mwakilishi wa BDG Tanzania Bara. Ofisi za Mikoa za SIDO ni vituo vya Wajasiriamali kupatia taarifa kuhusu BDG na kupatia msaada wa kuomba kushiriki katika Mashindano ya Mpango wa Biashara (BDP) au Mpango wa Kuendeleza Biashara (BDP). SIDO pia ni Mshirika Mkuu katika Programu ya utoaji mafunzo na ushauri.
SIDO website: www.sido.go.tz
Zanzibar National Chambers of Commerce, Industries and Agriculture ZNCCIA
Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima, Zanzibar (ZNCCIA) kinatoa mtandao wa wafanya biashara Zanzibar kushirikiana. ZNCCIA imesambaa katika Mikoa yote 5 ya Zanzibar. ZNCCIA ni mwakilishi wa BDG huko Zanzibar. Hivyo, ZNCCIA inatoa taarifa za hapo kwa hapo kuhusu BDG na Programu zake mbili (BPC na BDP) kwa Wajasiriamali wanaopenda na inawasaidia katika kujaza fomu za maombi katika mojawapo ya Programu hizi. ZNCCIA itawasimamia Wakufunzi na Washauri wote watakohusika na BDG.
ZNCCIA website: www.znccia.com





