
Karibu katika Business Development Gateway (BDG)
Programu ya Kufanikiwa Kibiashara (BDG) inawasaidia Wajasiriamali wa Tanzania kufanikisha biashara zao. Jambo moja zuri katika BDG ni kwamba si tu inazilenga biashara zilizosajiliwa, bali pia biashara zisizorasmi na zisizosajiliwa. Jambo lingine zuri ni kwamba BDG itaendeshwa kote nchini Tanzania ambapo Wajasiriamali wote watafaidika, wawe wanaendesha biashara zao Dar es Salaam, Rukwa, Lindi au Zanzibar.
Programu zetu
BDG itakuwa ni kituo kitakachotoa mafunzo na ushauri, sehemu ya kupata mahusiano ya kibiashara na mtaji kwa ajili ya mawazo muafaka ya biashara. Mtaji wa fedha utatolewa kwa Wajasiriamali watakaoshiriki kwa mafanikio katika mojawapo ya Programu mbili za BDG: Mpango wa Mashindano ya Biashara (BPC) kwa biashara zilizosajiliwa na Programu ya Kuendeleza Biashara (BDP) kwa biashara ndogo na/au zisizorasmi. Iwapo unapenda kushiriki, bonyeza kifungo kimoja kulia.
BDG ni juhudi za Serikali ya Tanzania zinazosimamiwa na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na kuendeshwa na Taasisi ya ICON kutoka Ujerumani.









